Habari

Imewekwa: Nov, 08 2018

BODI YA UTALII YAMKABIDHI MISS TANZANIA VIPEPERUSHI VYA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

News Images

Kama mnavyofahamu kuwa shindano la Miss Tanzania ni shindano maarufu na kubwa la urembo hapa chini ambalo huanzia chini katika ngazi ya mkoaikuatiwa na kanda na baadae ngazi ya Taifa ambapo mshindi wa kwanza wa shindano hili huiwakilisha nchi katika shindano la Miss World

Kwa kutambua hilo Bodi ya Utalii Tanzania imekuwa kwa nyakati tofauti wakati shindano hili likiendeshwa na kampuni ya LINO International ya Bw. Hashimu Lundega, ikidhamini na kushiriki kwa namna mbalimbali kusaidia kufanikisha shindano hili ikiwa ni pamoja na kutoa semina zinazohusu Utalii na vivutio vya utalii kwa ujumla, kusaidia safari za kuwapeleka warembo wanaoshiriki shindano hili katika maeneo ya vivutio vya utalii. Na mmoja wa washindi alikuwa akipewa heshima ya kuwa Miss Domestic Tourism.

Mwaka huu pia Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi zake za ikiwemo Bodi ya utalii Tanzania tulidhamini pia shindano hili ambalo safari hii liliendeshwa na kampuni ya “The Look” chini yaBi Basila Mwanukuzi.Pamoja na udhamini wa fedha tuliwaandalia pia ziara mbili za kitalii. Ziara ya kwanza iliyofanyika kabla ya shindano ilikuwa ni ya kutembelea hifadhi yam situ wa asili wa Amani Muheza Tanga na ziara ya pili ya kutembelea pori la akiba la Selous. Aidha Washiriki wa shindano hili walifanyiwa semina maalumu kuhusu utalii na vivutio vya utaliii.

Lengo la ziara na semina hiyo ilikuwa ni kuwajengea warembo wetu ufahamu na uelewa angalau kwa uchache kuhusu dhana ya utalii na vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini.

Tofauti na mashindano yaliyopita ya Miss Tanzania, mwaka huu washindi watanowalipewa hadhi na majukumu mengine ya kiutalii. Mshindi wa kwanza ambaye ni ndiye Miss Tanzania Bi Queen Elizabeth Mkune alipewa hadhi ya kuwa Miss Domestic Tourism na tafanya kazi hiyo chini ya uratibu wa TTB, mshindi mwngine miongoni mwa hao watano amepewa hadhi ya kuwa Miss Ruaha National Park na tafanya kazi chini yauratibu wa TANAPA, mshindi mwingine alipewa hadhi ya kuwa Miss Ngorongoro, mwingine Miss Selous na mwingine Miss Nature and ecology.

Kwa ujumla hawa wote watakuwa na majukumu ya kuyatangaza hayo maeneo waliyopewa. Kwa upande wa Bi Queen Elizabeth jukumu lake kubwa ni kushirikiana na sisi katika kutangaza utalii wa ndani kwa maana ya kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii kwa watanzania na kuwahimiza kuvitembela vivutio vyetu hivyo. Kazi hiii kama nilivyosema ataifanya kwa kushirikiana na sisi.

Ni kwa kuzingatia hilo ndiyo maana leo amefika hapa kutuaga akielekea kuiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss World litakalofanyika nchini China . Mrembo wetu anatarajia kusafiri kesho tarehe 8/11/2018 na atakuwa huko kwa mwezi mmoja mpaka siku ya kilele cha shindalo hilo litakalo fanyika tarehe 8/12/2018

Kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania napenda nichukue fursa hii kumtakia kila la heri na ushindi katika shindano hilo na pamoja ya kwamba yeye pia ni Miss Domestic Tourism lakini kwa kutambua kuwa atakapokuwa huko China atakutana na washiriki wengine kutoka mataifa mbalimbali tumeona ni vema pia tumkabidhi baadhi ya vielelezo vya utalii ili akavitumie kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii kwa washiriki na watu kutoka mataifa mbalimbali.Ni matumaini yetu makubwa kuwa ataifanya kazi hii vizuri na kwa uzalendo mkubwa, lakini tuna imani kubwa kuwa atafanya vizuri sana katika shindano hili na hasa ikizingatiwa kuwa Queen Elizabeth anayo rekodi nzuri sana katika mashindano ya urembo kwani mtakumbuka vizuri kuwa mbali ya kuwa Miss Tanzania anashikilia pia taji la mshindi wa kwanza la Miss World University Kundi la Afrika alilolinyakua huko Cambodia mwaka jana 2017.