Vitengo

Kitengo hiki kwa bodi ya Utalii kinahusika na mambo yote yanayohusiana na sheria

Kazi za Kitengo cha TEHAMA ni kuandaa, kutekeleza na kusimamia mifumo yote ya TEHAMA ambayo inalisaidia shirika kutimiza majukumu yake. Kitengo hiki pia kinasimamia matumizi ya vifaa vyote vya TEHAMA, kutoa msaada kwa watumiaji pamoja na kufanya matengenezo ya mifumo na vifaa vyote vya TEHAMA.

Ni kitengo ambacho kazi zake ni pamoja na kuhakikisha wadau wa nje na ndani wanakuwa na mtazamo chanya kwa shirika na piia kua kuwa na mahusiano mazuri baina yaa shirika na vyombo vya habari.

kitengo kinahusika na kufuatilia taratibu na sha shughuli zote zinazofanywa na TTB zinafuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Kitengo kinafanya majukumu yafuatayo;

a) Kushauri Menejimenti kwenye masuala yanayohusu ununuzi;

b) Kusimamia ununuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali;

c) Kuratibu vikao vya Bodi ya Zabuni ya Shirika;

d) Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni ya Shirika;

e) Kutayarisha Mpango wa Ununuzi (Procurement Plan) wa OR-MUU na RCIP;

f) Kuandaa orodha ya mahitaji ya wizara (statements of requirements);

g) Kuandaa nyaraka za zabuni;

h) Kuandaa matangazo ya zabuni na kutangaza zabuni mbalimbali;

i) Kuandaa mikataba ya ununuzi;

j) Kutunza kumbukumbu zote za ununuzi;

k) Kuandaa taarifa mbalimbali kwa mujibu wa sheria ya ununuzi wa umma; na

l) Utunzaji wa vifaa na kuratibu ufutaji wa vifaa chakavu (disposal of public assets).